
Chombo alikuwa miongoni mwa watu waliokamatwa na jeshi wakati lilipochukua madaraka kabla ya kujiuzulu Mugabe wiki hii.
Wakili wa Chombo, Lovemore Madhuku amesema mteja wake alikuwa amelazwa hospitali hapo jana akiwa na majeraha yaliyotokana na kipigo alichopigwa na jeshi akiwa kizuizini.