Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Waziri Mkuu atoa tamko kwa wakimbizi

Ijumaa , 11th Aug , 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu.

Waziri Majaliwa ametoa onyo hilo leo wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora na kusema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa huo. 

"Taarifa nilizonazo zinaonyesha katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na matukio ya mauaji 35, ujambazi matukio 12, umiliki wa silaha nao unatisha. Yamekamatwa magobole 11, bunduki aina ya SMG saba na Mark Four mbili. Tulikamata pia risasi 714 za SMG zikiwa kwenye ndoo za mafuta na juu yake wamepaka mafuta ya mawese. Pia risasi mbili za Mark Four zilikamatwa," alisema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wakazi hao ambao baadhi yao wamepewa uraia na wengine bado ni wakimbizi waonyane wanapokutana kwenye vikao vyao kwa sababu matendo yao yanaikwaza Serikali ambayo iliamua kuwapa hifadhi.

"Ni vema mkikutana kwenye vikao vyenu muelezane na kuonyana, ninawasihi matukio haya myadhibiti la sivyo mtaharibu nia njema iliyoleta uwepo wenu.  Bunduki na risasi zinakuja kufanya nini wakati nyie mko maeneo salama? Mauaji ya nini?  Kama kuna tatizo limekupata, muone Mwenyekiti wa kijiji,  atakusaidia," alisisitiza Waziri Majaliwa.

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi yao ambao wamegeuka mawakala na wameanza kuwaleta ndugu zao bila kufuata utaratibu.

"Hatuzuii mtu kutembelewa na ndugu yake, lakini ni lazima mfuate taratibu. Tunataka tudumishe amani iliyopo nchini lakini pia tudumishe urafiki wa nchi zetu mbili za Burundi na Tanzania," alisema Majaliwa.

Kwa upande mwingine, Mbunge wa jimbo la Ulyankulu, Bw. John Kadutu amemuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la upatikanaji wa maji kwenye tarafa hiyo, pia aliomba wasaidiwe ili kata tatu za Kanindo, Igombenkulu na Milambo ziwezeshwe kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.  

HABARI ZAIDI

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe