Alhamisi , 16th Jun , 2016

Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mhe Ally Salum Hapi amesikitishwa na matukio ya ubakwaji na kulawitiwa kwa watoto na kuwaomba wazazi kushirikiana kwa pamoja kuripoti matukio hayo mapema ili yaweze kuchukuliwa hatua .

Kauli hiyo imetolewa leo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa ambayo kimkoa imeadhimishwa katika Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo Magomeni jijini Dar es salaam ambapo amewaomba wazazi kushirikiana kwa pamoja kuripoi matukio hayo mapema ili yaweze kuchukuliwa hatua

Aidha, Mhe. Hapi amewataka waliojenga kwenye viwanja vya michezo vya watoto kuhama mara moja kwani wanafanyia upelelezi kubaini viwanja hivyo sambamba na kuwataka wanaopiga muziki masaa 24 karibu na maeneo ya shule kuacha mara moja.

Halikadhalika amewataka walimu wote wenye tabia za kufunga mageti ya shule kwa kuwa wanafunzi wamechelewa waache tabia kwani mtoto ana haki ya kupata elimu watakao kaidi atawachukulia hatua za kisheria.