Jumatano , 27th Mar , 2024

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwakukutwa na katoni 523 za pombe bandia za vinywaji aina ya Smart Gin ambazo walikuwa  wakizisambaza katika manispaa ya Iringa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi

Akithibitisha kuwakamata watuhumia hao Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ACP ALLAN BUKUMBI amesema katika uchunguzi wa awali umebaini  watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa kimara Jijini Dar es Salaam wametengeneza bidhaa hizo kupitia kiwanda bandia cha kilimanjaro Wine ambacho uchunguzi unaendelea kubaini mahali kilipo.

Katika hatua nyingine pia kamanda Bukumbi amesema jeshi hilo pia linawashikia watu saba kwatuhuma  za kukutwa na mali  mbalimbali za wizi ikiwemo  pikipiki nne ,runinga aina tofauti sabufa na vitu vingine ambapo watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.