Jumatano , 12th Aug , 2020

Wavuvi katika soko la samaki la kimataifa la Feri Jijini Dar es Salaam wamelalamikia kanuni iliyopo kwenye sheria ya uvuvi ya mwaka 2020 ambayo inakataza uvuvi wa mchana.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina akiwasili katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam

Wavuvi katika soko la samaki la kimataifa la Feri Jijini Dar es Salaam wamelalamikia kanuni iliyopo kwenye sheria ya uvuvi ya mwaka 2020 ambayo inakataza uvuvi wa mchana.

Wavuvi hao wametoa malalamiko hayo mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ambaye amefanya ziara katika soko hilo leo asubuhi ambapo wametaka kuwepo na marekebisho ya kanuni ambazo zinawatenga wavuvi na haziendani na sera ya uchumi na kipato cha kati kwa wananchi.

Akijibu malalamiko ya wavuvi hao Waziri Mh. Mpina anesema, ''kimsingi sio kila sheria inayotungwa ina lenga kumsaidia mtu isipokuwa ni serikali na wavuvi kukaa chini na kuzungumza ili kuona ni namna gani wanaweza kufanya katika hilo''.