Ijumaa , 15th Jul , 2016

Lori lililokuwa limebeba milipuko na kujiingiza katikati ya umati wa watu na kufanya shambulizi lililosababisha mauaji ya watu wasio na hatia zaidi ya 80 nchini Ufaransa.

Waokoaji walipokuwa wakisaidia watu waliokumbwa na mkasa wa shambulizi katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa.

Shambulio hilo lilitokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa ambapo watu walikuwa katika maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille ambayo hufanyika kwa shamra shamra za hali ya juuu kila mwaka.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre amesema lori hilo liliendelea kutembea kilo mita mbili kabla ya polisi kumpiga risasi dereva.

Rais Francois Hollande ameitisha kikao cha dharura mjini Paris huku wa kazi wa eneo la maafa wakitakiwa kutulia majumbani.