
Moja ya aina ya Mihadarati aina ya Bangi
Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya kimataifa kuhusu mihadarati iliyotolewa jana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu (UNODC).
Ingawa idadi inaonekena kuwa kubwa UNODC inasema haijaongezeka sana katika miaka mine iliyopita ikilinganishwa na idadi ya watu duniani, hata hivyo ripoti hivyo inapendekeza kwamba idadi ya watu wanaochukuliwa kuwa wameathirika na dawa za kulevya imeongezeka sana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita.
Sasa kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna watu milioni 29 katika kundi hilo ikilinganishwa na takwimu za nyuma za watu milioni 27.
Pia ripoti inasema watu wengine milioni 12 wanajidunga sindano za dawa za kulevya na asilimia 14 kati yao wanaishi na Virusi vya Ukimwi, VVU.