Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Uledi Musa akiongea na wadau wa Biashara
Uledi amesema hayo jana katika Warsha ya kuboresha mazingira ya biashara kwa wadau na maofisa biashara wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo amesema urasimu huo unasababisha kudorora kwa mzunguko wa huduma kwa jamii na uchumi.
Aidha Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa ili kuondoa urasimu huo wameanzisha njia nyingie ya usajili ambayo itasaidia Wafanyabiashra kuanzisha biashara zao bila kubugudhiwa.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Matokeo Makubwa Sasa (BRN), katika Wizara hiyo Sekela Mwaisera amesema utafiti wa mwaka 2014 unaonyesha kuwa Tanzania inashika nafasi ya 119 katia nchi 189 katika mchakato wa haraka wa uanzishwaji wa biashara.