Alhamisi , 13th Aug , 2015

Watanzania waliopo vijijini na mijini wameshauriwa kutumia fursa adhimu na adimu ya ufugaji wa samaki kwani ni rahisi kuwatunza, gharama ndogo ya maandalizi ya mradi ambao unaingiza kipato kikubwa kwa haraka na kwa muda mfupi.

Hili ni bwawa la kuchimbwa chini, lipo katika kituo cha ufugaji wa samaki cha serikali kilchopo Kingolwira mjini Morogoro

Ushauri huo umetolewa na Ofisa Masoko wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Daud Mwalusamba alipokuwa akizungumza na east africa radio mara baada ya kumalizika kwa siku kuu ya wakulima nane nane kanda ya kusini iliyofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale,jijini Mbeya.

Mwalusamba ameelezea manufaa ya samaki katika biashara na maisha ya binadamu kama lishe huku akifafanua kuwa ni mradi unaoanza kuingiza kipato mara baada ya kutimiza miezi

Kwa upande wake Baraka Goebu ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ufugaji ameelezea namna ambavyo samaki anatakiwa kufugwa na kutunzwa hadi kuleta tija kwa mfugaji.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Riverbanks Fish Farm,Kenny Nyambacha ameelezea mradi huo utakavyozalisha ajira kwa vijana wanaume kwa wanawake na kwamba ni fursa pekee kwa watanzania kuitumia.