Alhamisi , 8th Feb , 2024

Wananchi wa kijiji cha Lulenge Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani wameiomba serikali kuwa jengea kituo cha afya kwani ni muda mrefu sasa hawana Zahanati ya kijiji na kuwafanya watembee umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Wananchi hao wanasema ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo imekuwa hadithi kwani ulianzishwa ujenzi ila muda sasa kituo hiko hakimaliziwi bado hali ni tete kitu ambacho kinawasikitisha na kwamba wapo mama wajawazito ambao wanajifungua kila siku ambao wanalazimika kutembea umbali mrefu wa km. 12 hadi Ubena mjini kufuata huduma hizo.

"Shida yetu kubwa ni Zahanati kwasababu wake wetu wanajifungulia nyumbani na wanashindwa kufika hospitali, juzi hapa mpaka mjukuu wangu tumempeleka Chalinze ambapo ni uzazi wa degedege yaani kajifungua njiani sasa kafika mtu hoi hoi, sasa tunaomba serikali mziangalie changamoto hizo, tunapata shida Lulenge hii." alisema Saidi Sanga, Mwananchi wa Lulenge

"Tuna kero nyingi kama ulivyosikia kama ulivyoona kero kubwa ya kwanza ndio hizo zingine zimeshatatuliwa lakini bado tuna changamoto ya Zahanati ambapo mpaka sasa imekuwa kama ni hadithi tuna miaka mingi hapa Zahanati imekuwa changamoto kwahiyo kilio chetu kikubwa miongoni ni hiyo pia ni kero kubwa, wakina mama wengi wanaopata shida kutoka na umbali mpaka kufika kwenye vituo vya afya ila kama serikali italiona hili tutashukuru sana. "Ally Rashidi - Mwananchi wa Lulenge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji Lukas Sultan yeye amekiri kuwepo kwa adha iyo ya kukosekana kwa Zahanati ambapo amsema tayari wamekubaliana kujenga Zahanati kwa kuanza kwenye kitongoji ambacho wananchi wakitongoji hicho hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

"Tumeanza mkakati tukakusanya matofali kama 2,800 na tumeanza kuweka saiti ambayo tayari tumesafisha kiwanja lakini bado nguvu ni ndogo ya kiuchumi kwahiyo tunahitaji serikali itie mkono wake angalau tuondokane na iyo adha ya huduma ya afya" alisema Lukas Sultan, Mwenyekiti wa Lulenge.