Simu
Wakizungumza na EATV wanawake hao wamesema kuwa ujenzi wa kituo hiko cha Afya utaenda kupanua huduma za uzazi pamoja na huduma zingine walizokuwa wakizipata kutoka katika zahanati pamoja na kupunguza gharama ya kusafiri kwenda Hospital ya Nyangao kwa ajili ya kupata huduma hizo huku wanaume nao wakigongea msumari changamoto wanazokabiliana nazo wake zao pindi wanapokuwa wajawazito.
Hayo yote yamejiri hii leo Oktoba 15 ikiwa Mataifa yote ulimwenguni yanaadhimisha Siku Wanawake Vijijini.