Baadhi ya miti ya asili iliyokatwa
Wanawake zaidi 100 wa jamii ya kimasai katika kijiji cha Matebete wilayani Mbarali mkoani Mbeya walikimbia makazi yao na kuishi porini kwa muda wa siku mbili wakipinga miti ya asili kukatwa katika makazi yao, na wameshutumu uongozi wa kijiji hicho kuhusika na hujuma hizo.
Wakizungumza kijiji hapo baadhi ya wanawake hao wamesema miti hiyo wameitunza kwa zaidi ya miaka 20, na walikuwa wanaendelea kuhifadhi kwa ajili ya familia zao na kizazi kijacho, miti hiyo imekatwa kwa ajili ya kupata mbao za madawati na kwamba walipojaribu kupinga sauti za wanawake zilipuzwa kwenye mkutano wa kijiji.
Kijiji cha Matebete kiko ndani ya hifadhi ya msitu ambao unamilikiwa na jamii ya wafugaji wa kimasai tangu miaka 40 iliyopita, ambapo baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali umetumia uelewa mdogo wa jamii ya wafugaji kupora miti hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha matebete bwana Iman tisho amekiri kukata miti hiyo hata iliyo katika makazi ya watu, amesema hatua hiyo ilishirikisha wananchi katika mkutano wa hadhara wa kijiji.
Naye Afisa Maliasili wa wilaya ya Mbarali bwana Kenedy Hincha akizumgumza kwa njia ya simu amekiri kukatwa kwa miti na kwamba ni kwa mjibu wa sheria