Wananchi waua wakiisaidia polisi

Wednesday , 11th Oct , 2017

Jambazi mmoja ameuawa na wananchi wakati akiwatoroka askari baada ya kubainika kufanya jaribio la kutenda uhalifu katika mradi wa ujenzi wa kituo cha pamoja cha forodha OSBP Tunduma mkoani Songwe.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa Songwe amesema tarehe 10 usiku wa kuamkia jumatano hii majambazi hao walipanga kufanya tukio la uhalifu katika mradi wa ujenzi wa kituo cha forodha OSBP

Tunduma na kwamba baada ya kugundulika walikimbia na kutelekeza bunduki yenye risasi 30, na zana zingine walizokuwa nazo.

Kamanda Nyange amesema majambazi wawili walifanikiwa kutoroka wakati mmoja aliyetajwa kwa jina la Isha Martin Mwampulo (20) mkazi wa Lwasho kata ya Ndalambo wilayani Momba akinaswa na wananchi, ambapo hata hivyo baada ya kushambuliwa alijeruhiwa vibaya na kufariki dunia akiwa njiani kuwahishwa hospitali.

Wakazi wa mji wa Tunduma mbali ya kupongeza jitihada za jeshi la polisi, wamesema wako tayari kushiriki kikamilifu katika kufichua wahalifu lakini wakataja kasoro ya askari kuchelewa kufika pindi wanapoarifiwa kuhusu uhalifu jambo linalowakatisha tamaa wananchi katika kushiriki kupambana na uhalifu.

Aidha jeshi la polisi limedai kuwa jambazi huyo alikuwa amevaa sare za wakandarasi na kutumia mwanya huo kutaka kutekeleza azma yake.

Kamanda nyange ameendelea kutahadharisha kuwa Mkoa wa S ongwe sio mahali salama kwa wahalifu na kupongeza ushirikiano wa wananchi kwa jeshi la polisi hadi hivi sasa