Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha wanahabari wanawake Tanzania-TAMWA- Valerie Msoka.
Akizungumza leo Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha wanahabari wanawake Tanzania-TAMWA- Valerie Msoka amesema kuwa wataendelea kufanya kazi na madawati ya jinsia,viongozi pamoja na jamii ili kutokomeza kabisa suala hilo.
Bi. Msoka amesema bado wanaendelea na harakati za kuhamasishawa wanawake juu ya kujua madhara ya ndoa hizo ambazo sehemu nyingi hasa vijijini zinatokana na maamuzi ya waume zao jambo linalowafanywa washindwe kupinga.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa Takwimu zinaonyesha kuwa watoto 8000 wanapata mimba wakiwa bado wapo shuleni na kati ya hao 3000 wapo chini ya umri wa miaka 18 hivyo juhudi za makusudi za pamoja zinahitajika ili kukomesha hali hiyo pamoja na kuwarejesha shuleni kuendelea kupata elimu.