Alhamisi , 8th Jul , 2021

Wanafunzi zaidi ya 400 wa shule ya msingi Ifwagi, iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, wapo hatarini kuugua magonjwa ya tumbo yakiwamo ya kuharisha kutokana na shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya vyoo, hali inayowalazimu baadhi yao kujisaidia ovyo vichakani.

Vyoo vya shule ya msingi Ifwagi

Mbali na changamoto hiyo, wanafunzi hao pia wanalazimika kutembea umbali wa kilometa tano kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi shuleni hapo, jambo linalowakosesha baadhi yao vipindi vya masomo darasani.

Aidha, wanafunzi hao wamelalamika kuwa hali ya upungufu wa vyoo imepelekea wao kuchelewa vipindi kutokana na uwepo wa foleni vyooni na kwamba wakati mwingine choo kisafi huwa ni kimoja na vingine vyote kuwa vichafu licha ya kusafishwa.