Jumapili , 23rd Jun , 2019

Wanafunzi watatu wa kike wa darasa la saba katika shule ya msingi Nyamalele wilayani Geita wamekamatwa katika nyumba wanayoishi wanafunzi wenzao wa shule ya sekondari ya Nkome.

Wanafunzi

Umri wa wanafunzi hao wa kike ni miaka 13 ambapo baada ya kutoroka nyumbani kwao, wamekutwa wakiishi kinyumba na wenzao wa kiume wa sekondari wenye umri wa miaka 16.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Kata ya Nkome, John Matanga, watoto hao wamekamatwa usiku wa kuamkia jana Jumamosi Juni 22, 2019 saa saba baada ya kuwatafuta kwa siku tatu kufuatia taarifa za wazazi kudai watoto wao wamepotea.

Matanga amesema wanafunzi hao walikamatwa kwenye nyumba ya Sophia Agustin ambaye mtoto wake wa kidato cha pili aliwakaribisha kuishi kwa siri katika chumba chake.

Amesema wanafunzi hao walikutwa wakifanya mapenzi, ambapo sasa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo ili iwe fundisho kwa wazazi wengine kutokana na kutowajibika vyema katika malezi.