Alhamisi , 4th Sep , 2025

Utawala wa Trump umekosoa vikali operesheni za kulinda amani ukishtumu kushindwa kwa misheni nchini Mali, DRC, na Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutaja mabilioni ya dola zilizotumika, miradi mikubwa ya ufisadi na ubadhirifu uliopo nyuma yake.

Umoja wa Mataifa unahofia kuathirika kwa shughuli za kulinda amani kufuatia kushuka kwa kasi kwa misaada ya maendeleo ya Marekani huku rais Donald Trump wa Marekani akifuta msaada wa dola bilioni 4.9 wa msaada wa kigeni ambao ulikuwa umeidhinishwa na Baraza la Congressjuma lililopita.

Dola milioni 800 kati ya msaada huo, zingefadhili shughuli za ulinzi wa amani duniani kote, nusu yake zikitengwa kwa bara la Afrika. Kulingana na Umoja wa Mataifa, hii inaweza kuhatarisha usalama wa raia, haswa nchini Sudan Kusini na DRC.

Utawala wa Trump umekosoa vikali operesheni za kulinda amani ukishtumu kushindwa kwa misheni nchini Mali, DRC, na Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutaja mabilioni ya dola zilizotumika, miradi mikubwa ya ufisadi na ubadhirifu uliopo nyuma yake.

Donald Trump pia ameushutumu Umoja wa Mataifa kwa kutumia pesa zilizotengwa kudumisha usalama kwa madhumuni mengine. Hivi sasa Umoja wa Mataifa unakabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi unaofikia dola bilioni 2.7 ili kufadhili shughuli za kulinda amani.

Marekani pia imekataa kufadhili, kupitia Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AUSSOM, ulioanzishwa kupambana na magaidi wa Al Shabaab. Operesheni hii bado inatafuta mpango thabiti wa ufadhili.