Jumapili , 21st Jul , 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameendelea na ziara yake mkoani Kilimanjaro ya kukagua miradi mbalimbali mkoani humo.

Akiwa wilayani Same, Waziri Mkuu amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Pauline Nkwama amsimamie Afisa Elimu wa Wilaya hiyo anayeshughulikia elimu ya msingi, kuhakikisha anawahamishia walimu kwenye shule mbili za Kirya zenye walimu wawili pekee, huku zikiwa na wanafunzi zaidi ya 400 kila moja.

Afisa Elimu Mkoa hakikisha Afisa Elimu wa elimu ya msingi katika wilaya hii anahamisha walimu kutoka pale mjini na kuwaleta huku ili huku vijijini kuwe na walimu sita katika kila shule. Kesho Jumapili (leo) andika barua za uhamisho, Jumatatu wapewe ili Jumanne waje kuripoti huku,” alisema. amesema Majaliwa.

Aidha akizungumza na wakazi wa Kirya, Nyumba ya Mungu na vijiji vilivyo jirani na eneo la mradi wa maji, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutoa fedha hatua kwa hatua ili kukamilisha mradi huo na kuwataka wakazi hao waache kutumia uvuvi haramu na badala yake, wavue samaki kwa kutumia njia halali.

Bwawa la Nyumba ya Mungu linagusa wilaya tatu za Mwanga, Simanjiro na Moshi Vijijini. Ninataka Serikali za wilaya husika zisimamie jambo hilo”.