Alhamisi , 16th Jul , 2015

Wakulima wa mkonge wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamekata tamaa na kuamua kuachana na kilimo cha zao la mkonge kutoka na kushuka kwa bei na kuomba serikali kusaidia kupata bei nzuri za mkonge ili kufufua kilimo cha mkonge.

Moja ya Mazao yatokanayo na Zao la Mkonge.

Wakizungumza huku wakionesha mashamba ya wazi baada ya kuachana na kilimo cha mkonge wakulima hao wameeleza walivyokata tamaa na kilimo hicho kutokana kushuka kwa bei huku wakitumia gharama kubwa za uzalishaji ikilinganishwa na bei ndogo za zao la mkonge.

Aidha wakulima hao wameomba serikali kuboresha bei katika masoko ili kurudisha imani kwa wakulima kurudi katika kilimo cha amkonge ambacho walikitegemea katika kuongeza pato la kaya.

Naye mratibu wa utafiti kanda ya mashariki kwa kushirikiana na usimamizi wa viwanda vidogo nchini SIDO, Adriani Biza amesema zao la mkonge lilikuwa ni zao linategewa na wananchi wa kilosa lakini kutokana kushuka thamani wakulima wamekata tamaa kuendelea kulima.

Amesema imefika wakati wa serikali kuinua zao hilo na kumsaidia mkulima ambapo sido wamahidi kusaidia upatikana na viwanda vidogo vya kusaidia kusokota mkonge ili wafufue kilimo cha za zao mkonge.