Ofisa Wanyamapori wilaya ya Sengerema Paul Poncian amesema Matukio haya ni kuanzia Julai 2023 hadi hadi April 2024
Watu wanaoathirika kwa kupoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba ni wavuvi sambamba na watu wanaokwenda kuteka maji ,kuosha vyombo, kufua na kuoga ndani ya ziwa Victoria.
Hindigai Marwa, Jackisoni Rock wakazi wa Kijiji cha Izindabo Kata ya Lugata kisiwa cha Kome na Mabohele Gabriel mkazi wa Kata Nyakasasa ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa na mamba wakati wakifanya shughuri za kibinadamu ndani ya ziwa Victoria.
Huku Magesa Kapanda. Mkazi wa Kijiji cha Bulyaheke, na majani Nyambabi mkazi wa Kijiji cha Kahuda ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba walipokuwa wakifanya shughuli za kibinadamu ndani ya ziwa Victoria
Baadhi ya wananchi wa Buchosa wameiomba Serikali kuweka kituo kidogo cha Tawa Buchosa ili kirahisha watu kupata huduma mapema yanapotokea matukioa ya wananchi kushambuliwa na mamba .
Amos John mkazi wa Bukokwa amesema watu waliotoza maisha kwa kushambuliwa na mamba ni idada kubwa ambayo Serikali inatopeza nguvu kazi.
"Watu niwengi waliopoteza maisha kwa kipindi cha miaka miwili hivyo jitihada za haraka zinatakiwa kuwanusuru watu wengine ,amesema John.
Kwa Halmashauri ya Sengerema watu walioli poteza maisha kwa kuliwa na mamba 19 huku 20 wakijeruhiwa kuanzi mwaka 2019 had march 2024.
Poncia alitaja mkakati wa Serikali kupitia wizara ya maliasi na utalii ni kujenga vizimba maeneo hatarishi ambavyo vitasaidi watu kutokushambuliwa na mamba.