Jumatatu , 12th Sep , 2016

Waislam duniani kote leo wanasherehekea sikukuu ya Eid El-Hajj mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Hijja ya kila mwaka inayotekelezwa na waisilamu duniani kote waliposimama katika mlima wa Arafat Magharibi mwa Saudi Arabia.

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi.

Swala ya Eid El Hajj kitaifa nchini Tanzania imefanyika asubuhi hii katika viwanja vya Baraza Kuu la Waislam Tanzania, BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Baraza la Eid litafanyika mara baada ya swala ya Eid na mgeni rasmi wa baraza hilo asnatarajiwa kuwa ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zuberi.

Inakadiriwa kuwa waisilamu wapatao milioni moja na laki nane walikusanyika na kuuzunguka mlima huo tokea majira ya alfajiri jua lilipopambazuka.

Kila muisilamu mwenye uwezo na afya njema analazimika kutekeleza ibada ya Hijja angalau mara moja katika uhai wake.

Kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa, idadi kamili ya mahujaji mwaka huu ilikuwa ni watu milioni moja na laki nane na milioni moja na laki tatu kati yao wametoka nchi za nje ya Saudi Arabia.