Wahamiaji haramu waliowahi kukamatwa nchini
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha
Amesema inashangaza kuona silaha za aina nyingi katika maeneo mbalimbali ambazo Tanzania hakuna ambazo zinadaiwa kuingia nchini kupitia maeneo ya mpakani. “Hivyo ni lazima Idara ya Uhamiaji ihakikishe wanadhibiti uingiaji wa wahamiaji kwenye mipaka mbalimbali nchini,”.
Waziri Mkuu amesema Serikali haizuii wageni kutoka mataifa mengine kuingia nchini ila ni lazima udhibiti wa wageni hao ufanyike ikiwa ni pamoja na kujiridhisha sababu za kuja nchini na muda watakao kuwepo.
Hata hivyo aliwasihi watumishi wa idara mbalimbali za Serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa nidhamu, weledi, uadilifu na kuwatumikia wananchi wanaohitaji huduma mbalimbali hata kama wamekosea kuuliza katika maeneo yao.
Amesema “baadhi ya wananchi hawana uelewa juu ya wapi wapeleke malalamiko yao lakini kwa kuwa wewe ni mtumishi wa umma unapaswa kumsikiliza na kumwelekeza aende wapi badala ya kumtolea maneno yasiyofaa,”.





