
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa utoaji elimu na huduma ya upimaji kwa wananchi Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwa siku taasisi hiyo inapokea wagonjwa zaidi ya 300 huku akitoa tahadhari zaidi kuhusu mtindo wa maisha.
Amesema kuwa kila mwaka duniani kote zaidi watu 18,000 hufariki dunia kutokana na magonjwa ya moyo huku katika kila kina mama wanne mmoja anatatizo la shinikizo la moyo na wakinababa watano mmoja ana tatizo hilo na kushauri matumizi sahihi ya dawa na ufanyaji wa mazoezi.
"Hiyo ni karibu asilimia 31 ya ugonjwa wa moyo, mwaka huu dunia nzima inaeleza kuwa magonjwa yanakinga na kinga yake ni nzuri zaidi kuliko matibabu ikiwemo kufanya mazoezi, ambavyo vinaweza kufanywa kwa gharama nafuu" alisema Prof Janabi