Jumatatu , 4th Jan , 2016

Jamii ya wafugaji Mkoani Tanga imetakiwa kutumia fursa ilitolewa na serikali ya awamu ya tano ya kusitisha michango na ada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuwapeleka watoto wa shule badala ya kuwatumikisha katika kazi za uchungaji.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Hajat Mwamtum Mahiza.

Akizungumza na Wafugaji wilayani Handeni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Hajat Mwamtum Mahiza amewataka viongozi wa kata kuwahimiza wazazi kuwaandikisha watoto shule ili azma ya Serikali iweze kufikiwa.

Bi. Mwamtumu amesema ili kuweza kufuga kwa tija ni lazima mtoto apate elimu hivyo wazazi hawana budi kuwapeleka watoto shule badala ya kuwaachia kundi kubwa la mifugo ambayo mara nyingi huwashinda nguvu na kusababisha migogoro.

Bi Mwantumu amesema kuwa baada ya mtoto kumaliza elimu ya Msingi au sekondari endapo atapenda kuwa mfugaji basi mzazi amuachie afanye hivyo lakini baada ya kuhakikisha amepata elimu ya kumuwezesha kuendeleza mifugo hiyo.