Jumanne , 2nd Aug , 2016

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaam imewataka wafanyabiashara kuzingatia muda uliopangwa na Serikali kwa ajili ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi unaofanywa kila ifikapo siku ya jumamosi.

Wafanyabiashara wa mboga mboga katika Soko la Ilala Boma, wakiuza mbogamboga katika eneo ambalo Si salama kwa afya ya mlaji

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaaam imewataka wafanyabiashara kuzingatia muda uliopangwa na Serikali kwa ajili ya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya kazi unaofanywa kila ifikapo siku ya jumamosi.

Muda uliowekwa kwa ajili ya zoezi hilo ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:30 asubuhi,Kila siku ya Jumamosi ambapo wafanyabiashara wote watapaswa kufungua maduka na masoko yao mara baada ya zoezi hilo kukamilika.

Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa wa Manispaa hiyo, David Langa kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya zoezi la usafi wa mazingira Wafanyabiashara wenye tabia ya kuchelewa ili wafike baada ya muda wa usafi pamoja na wale wanaofungua biashara kabla ya muda uliopangwa na Serikali waache mara moja

Langa ameongezakuwa wananchi wanaopenda kutupa taka hovyo kuacha mara moja vinginevyo sheria ya afya na sheria ya mazingira inapinga suala hilo na kwa mujibu wa sheria hizo adhabu yake ni faini ya shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miaka 6 jela.