Mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika Kasunga.
Muuguzi msimamizi wa wodi ya watoto katika hospitali ya Mount Meru Sister Rosemery Mashauri amesema awali watoto wanaozaliwa kabla ya wakati hospitalini hapo walikuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza kutokana na kulazimika kulala wanne hadi sita katika kitanda kimoja tofauti na sasa ambapo kila mtoto analala katika kitanda chake.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika Kasunga aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa mwito kwa wadau wengine kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za Afya kwa wananchi huku Mkuu wa Wodi ya Watoto Hospitalini hapo Dakta Mariam Muqtaz akieleza msaada huo kama mkombozi mkubwa katika idara hiyo.
Sehemu ya ufadhli huo ni pamoja na vifaa maalumu vya kuhifadhi watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati,makabati kwa ajili ya kuhifadhia vifaa vya wagonjwa na dawa pamoja na kukarabati jengo la wodi ya watoto Njiti hospitalini hapo.