Jumamosi , 11th Mar , 2023

Wachimbaji wadogo 8 wa Madini ya Dhahabu wanaofanya uchimbaji katika kijiji cha Igando kata ya Magenge wilaya ya Geita wamepoteza maisha baada ya shimo walilokuwa wakichimba kujaa Maji

Maji hayo yanatokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Geita

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo vilivyotokea usiku wa kuamkia leo March 11, huku akisema kuwa eneo hilo lilikuwa limefungiwa uzalishaji kutokana na sababu za kiusalama