Jumanne , 28th Aug , 2018

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai, amethibitisha kuwa wabunge wawili ambao ni Hawa Ghasia na Jitu Soni kwa pamoja wamejiuzulu nafasi zao kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti.

Kushoto ni Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) Hawa Ghasia na kulia ni mbunge wa Babati Vijijini (CCM) Jitu Soni.

Kagaigai amesema amepata taarifa za kujiuzulu kwa Hawa Ghasia, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti na Jitu Soni ambaye ni Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

''Ni kweli wamejiuzulu lakini mpaka sasa sijapata sababu za wao kufanya hivyo lakini taarifa ya kujiuzulu ni kweli tunachosubiri ni wenyewe kuweka wazi sababu zilizolekea wakae kando'', amesema.

Ghasia ambaye ni mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) na Soni ambaye naye ni Mbunge wa Babati Vijijini kupitia (CCM), wametangaza uamuzi wao huo leo asubuhi mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati hiyo.