
Akijibu Mwongozo huo Naibu Spika Tulia Ackson amesema kwa kuzingatia kanuni za Bunge ibara ya 46 (1) inayomtaka kila Mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge na kutimiza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi hivyo kitendo cha wabunge kuingia Bungeni na kujisajili na kutoka nje ni kukiuka kanuni za Bunge.
Naibu Spika ametoa mwongozo kwa kurejea miongozo mingine ya kiti ambayo iliwahi kufanyika hapo awali akigusia mfano wa tarehe 08 April mwaka 2008 ambapo wabunge wa Chama cha CUF waligomea vikao na Bunge kupendekeza wabunge hao wakatwe posho.
Kwa kurejea kanuni hiyo ya 146 (1) ambayo inawataka wabunge kuhushuria vikao, kwa kutohudhuria kwao na kuchukua posho ni jambo ambalo halikubaliki hivyo kuanzia sasa wabunge ambao wamesusia vikao vya bunge watakatwa posho zao zote kuanzia walipoanza kususia vikao.