
Kikao hicho kitaanza kwa kusomwa kwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli la kuitisha Bunge hilo na baada ya kusomwa kwa tamko hilo, kutafuatiwa na uchaguzi wa Spika ambao utafanyika kwa siri.
Ratiba hiyo inaonesha Spika atawaapisha wabunge wa bunge hilo la muungano kwa siku mbili, ambapo siku ya Alhamisi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwasilisha jina la waziri mkuu ambalo litasomwa mbele ya wabunge wote na kuthibitishwa kwa kupigiwa kura.
Rais Magufuli anatarajia kulihutuibia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Ijumaa saa kumi jioni ikiwa ni hotuba yake ya kwanza ya kulifungua rasmi Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.