Jumatatu , 26th Jun , 2023

Wabunge wa bunge la Tanzania wameidhinisha bajeti ya Sh44.39 trilioni kwa mwaka wa fedha 2023/2024 

Katika kura zilizopigwa leo Juni 26/2023 wabunge 354 wamepiga kura za ndio, wabunge ambao hawakuwa na uamuzi ni 20 na kura za hapana ni sifuri huku wabunge 18 hawakuwepo bungeni

Kabla ya kupigiwa kura na wabunge Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amejibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wabunge ikiwemo tozo ya shilingi mia moja katika nishati ya mafuta

"Serikali inafanya ufuatiliaji wa ndani kuhusu soko la dunia kwenye masuala ya nishati ya mafuta, tena watanzania hata msiwe na hofu na hii shilingi 100, kwa sababu kuna wakati mafuta yalipanda kwenye soko la dunia sio hata kwa ajili ya shilingi 100 serikali ikaweka ruzuku" amesema Nchemba

Aidha amewashangaa wanaowaza kuhusu uchaguzi wa mwaka 2025 huku akisema kwa miradi inayotekelezwa na serikali haoni haja ya kuwaza uchaguzi ujao

"Kwa wale wengine wote wanaojadili kuhusu 2025, ndugu zangu nimewatajia miradi yote na mambo ambavyo yameongezeka kwa kiwango cha mvua ile ambayo hamuwezi kuonana nayo, kwa kiwango cha mafuriko, unajadilije kuhusu uchaguzi"