Jumapili , 10th Dec , 2023

Vijana wawili ambao ni ndugu wa familia moja Zephania Tinkson Mdolo (20) na Kelvin Tinkson Mdolo (17), wamedai kukatwa vidolegumba vya miguu na mtu aliyefahamika kuwa ni balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mpemba Mjini Tunduma mkoani Songwe kwa kuwatuhumu kuwa ni wezi.

Vijana waliokatwa vidole gumba

Wakizungumzia tukio hilo lililotokea tarehe 03 Nov vijana hao wanadai tarehe hiyo walikuwa kuchunga mifugo ndipo balozi aliwaita na kuwakata vidole na kuwabebesha Nondo akidai kuwa ni wezi wa Nondo.ZEPHANIA MDOLO M

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Songwe ACP Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanamshikilia Samwel Eckson Mnkondya, anayedaiwa kuwa ni balozi, kwa tuhuma za kuwakata vidole vijana hao.