Vijana wakiwa Internet kutafuta mambo mbalimbali
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Meneja Matukio, wa Buni Inovation Hub, katika tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),Mariam Mgonja, amesema mitandao ya kijamii ina fursa nyingi zinazowahusu vijana ikiwemo teknolojia ya biashara katika jamii.
Bi. Mgonja amesema kuwa vijana wengi wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kifanya mambo ambayo hayanamsingi katika maendeleo yao ya kila siku kiuchumi hali inayowafanya kushinda kujiendeleza katika kujitafutia kipato.
Vijana wawili wa kitanzania wametumia mitandao kikamilifu na kufanikiwa kuingia katika fainali ya Mashindano ya Afrika Busness Cup, yanayojumuisha nchi tano za Afrika kuhusu teknolojia na biashara mitandaoni.
Meneja wa Bmm Afrika Alex Kapungu amesema washiriki hao mmoja alitumia vifaa vya kieletroniki ambavyo vikitumika vinakua havitumiki hivyo ameanzanisha mradi wa kufanya recyclin na mwingine amebuni mradi wa kutengeneza Pedi zinatakotumia muda mrefu.





