Waziri wa Kilimo Hussein Bashe
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akitoa maelezo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alizindua mradi huo na kuwapatia baadhi ya vijana hao vitendea kazi.
"Kwa hiyo vijana 420 kutoka nchi nzima ikiwamo Zanzibar utawakabidhi vitendea kazi wawakilishi wao ambao watafanya kazi na mkulima kuwatengenezea vihenge na kuwauzia. Itakuwa ni sehemu ya ajira kwao hasa ikizingatiwa ni vijana waliopewa mafunzo na serikali na wamepewa vifaa vya kutengenezea vihenge hivyo," amesema Waziri Bashe
Akifafanua kuhusu mradi huo wa sumukuvu, Bashe amesema serikali imeshirikiana na watalaam wa VETA, Wizara ya elimu kuwapatia mafunzo vijana hao 420 namna ya kutengeneza vihenge.