ACP Thobias Sedoyeka
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Thobias Sedoyeka, amesema kikundi hicho kilichoweka kambi katika kijiji cha Chiwindi kata ya Mcholi II tarafa ya Mkunya wilayani Newala, kinaundwa na vijana zaidi ya 25, huku waliokamatwa wote ni wakazi wa Newala, wakipatiwa mafunzo na vijana walioshiriki vikundi vya Panya Road vya Dar es Salaam.
Aidha, kamanda wa polisi amesema katika msako walioufanya, wapo baadhi ya watuhumiwa hawakuweza kukamatwa, huku wale waliokamatwa wameeleza lengo la kikundi chao kuwa ni kuunda umoja wenye nguvu ya kufanya uhalifu.
Katika hatua nyingine, Sedoyeka ametoa taarifa ya hali ya uhalifu mkoani humo kuanzia mwezi Januari mpaka Novemba mwaka jana, ambapo ajali zilizosababisha vifo zikiongezeka kwa asilimia 10 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2015.
Msikilize hapa Kamanda Sedoyeka




