
Waziri Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akiangalia vipeperushi katika viwanja vya Majimaji Songea.
Hilo limewekwa bayana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua Kampeni ya FURAHA YANGU, PIMA, JITAMBUE, ISHI katika viwanja vya Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma.
“Wataalam wa Afya na Wanasayansi wamethibitisha kwamba mtu akianza mapema kutumia dawa za ARV anapunguza vitu vingi sana vinavyoweza kudhuru afya yake na ya wengine ikiwemo uwezekano wa kupata magonjwa nyemelezi pamoja na uwezekano wa kuwaambukiza wengine” amesema Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy amesema Takwimu za Kitaifa zinaonesha maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 4.7, huku bado maambukizi mapya yakiendelea kuwepo hususani kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.
Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa asilimia 52 ya watu wanaoishi na maambukizi ya VVU wanajifahamu kuwa wana VVU wakati katika kila watu 100 watu 48 wenye maambukizi ya VVU hawajui kuwa wana VVU jambo ambalo ni hatari kwao na Taifa kwa ujumla.