Ijumaa , 17th Jun , 2016

Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sekta ya utalii imelalamikiwa na Muungano wa vyama vya Waongoza Watalii nchini (TTGA) kuwa itadhoofisha sekta hiyo.

Katibu wa Muungano huo Emanuel Mollel amesema wamekuwa wakikaa na watalii kwa asilimia 90 baada ya kufika nchini wamekuwa wakilalamika juu gharama kubwa za kuja kutalii nchini kutokana na tozo mpya ya VAT.

Alisema kuwa mojawapo ya changamoto wanazopata watalii ni pamoja na kutokuwepo na ndege ya moja kwa moja, na kuwa mtalii anapoingia nchini hutakiwa kulipa tozo ya dola elfu 7 hadi elfu 10 hivyo kuongeza VAT katika huduma za watalii kutawakimbiza watalii hao.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti TTGA Khalifa Msangi alisema kuwa serikali kabla ya kutaka kuanzisha kodi hiyo ilipaswa kuwashirkisha wadau lakini haijafanya hivyo hali ambayo itazua mgogoro mkubwa na kuzorotesha mapato yatokanayo na sekta ya utalii.