Jumanne , 27th Sep , 2016

Utafiti uliofanywa na taasisi inayojishughulisha na utafiti wa jinsi ya kupunguza umaskini ya REPOA umebaini kushuka kwa idadi ya viwanda vya utengenezaji dawa za binadamu nchini.

Dkt. Richard Katera

Utafiti huo umeonesha kuwa hali hiyo imetokana na uwekezaji mdogo kwenye sekta hiyo ambao kwa sasa inaonekana haitengenezi faida.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REPOA Dkt Lucas Katera amesema hayo leo wakati akitoa matokeo ya utafiti huo uliolenga kutoa ushauri wa jinsi ya kufufua sekta ya utengenezaji wa dawa nchini, sekta ambayo miaka ya themanini na tisini ilikuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi.

Kuhusu nini kifanyike kuongeza uwekezaji kwenye viwanda vya dawa nchini, Dkt Katera amesema kuna haja ya serikali kuangalia eneo la ushindani, sera ya uendelezaji viwanda vya ndani pamoja na upatikanaji wa nishati ya uhakika, vitu ambavyo amesema vimekuwa vikichangia hasara kwenye viwanda vya dawa.