Kiongozi wa Chama Tawala cha Afrika Kusini ANC,Jacob Zuma
Ingawa chama tawala cha ANC kinaongoza kwa matokeo yaliyotolewa hadi sasa lakini bado kinaonekana kuzidiwa na chama cha Democratic Alliance katika mji wa Port Elizabeth.
Aidha chama cha ANC huenda kisifikie asilimia 50 ya kura katika miji ya Pretoria na Johannesburg.
Wakati asilimia 85 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa nchini kote chama cha ANC kinaongoza kwa asilimia 53 kikifuatiwa na chama cha Democratic Alliance ambacho hadi sasa kina asilimia 27 huku chama cha Economic Freedom Fighters kikipata asilimia 7.5 ya kura hizo.
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa yanatarajiwa kutangazwa leo.