Jumatatu , 12th Mei , 2014

Kambi ya upinzani bungeni imesema mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanayotokana na misaada na mikopo ya wahisani wa nje, Zanzibar hupewa asilimia ndogo ya mapato hayo kutokana na asilimia kubwa kutumika Tanzania Bara.

Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tundu Lissu.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Kambi hiyo, Mhe. Tundu Lissu wakati akitoa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani Bungeni, katika kikao cha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Mhe. Lissu amesema katika mwaka wa fedha uliopita mapato halisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yalikuwa trilioni 1.63 ambapo Zanzibar ilitakiwa kupewa bilioni 52.33 badala yake ilipewa bilioni 33.8 ambazo ni pungufu.