
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho
Utafiti ambao umefanywa na tume ya taifa ya kudhibiti ukimwi, tacaids, umebaini kuwa kasi ya maambukizi ya ukimwi kwa vijana wa kike mkoani mbeya ni kubwa ikilinganishwa na vijana wa kiume.
Akizungumza na chombo hiki mratibu wa ukimwi mkoani mbeya, stella kategile ameeleza sababu ya kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa mtoto wa kike mkoani mbeya kuwa juu ikilinganishwa na mtoto wa kiume
Kwa mujibu wa takwimu za kitaifa, mkoa wa mbeya unashika nafasi ya tatu kwa kuwa na maambukizi makubwa ya ukimwi nchini, ukitanguliwa na mkoa wa dar es salaam na iringa.