
Akizungumza katika kikao cha Makamishna wapya wa tume hiyo jana jijini Dar es salaam Dakta Maboko amesema watanzania wasuidanganyikwe na kudhani kuwa ukimwi umekwisha na kuwataka wanainch kuendelea kupima kila wakati ili kujiepusha na maambukizi mapya.
Amesema takwimu zinaonyesha kuwa baadhi ya mikoa ya nyanda za juu kama Iringa na Njombe idadi ya waadhirika bado ni kubwa tofauti na mikoa mingine na kuainisha kuwa hiyo ni kutokana na watu wengi kudharau kupima kila wakati.
Dakta Maboko ameainisha kwamba mpaka sasa Tanzania Bara ina maambukizi ya asilimia 5.3 sawa na watu milioni mbili wakliopata maambukizi.