Jumamosi , 2nd Dec , 2023

Matetemeko mawili makubwa ya ardhi yamepiga kisiwa cha pili kwa ukubwa nchini Ufilipino cha Mindanao, na kusababisha hofu ya awali ya uwezekano wa "uharibifu wa tsunami''

 Utafiti wa Jiolojia wa Marekani ulipima tetemeko la kwanza siku ya Jumamosi kwa ukubwa wa 7.6, na lile lililofuata muda mfupi baadaye saa 6.4.

Taasisi ya Volcanology na Seismology ya Ufilipino imesema tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 6.9 na 6.4.Mfumo wa tahadhari ya tsunami nchini Marekani baadaye ulisema kuwa tishio la tsunami "limepita".

"Kupungua kwa kiwango cha bahari kunaweza kutokea katika baadhi ya maeneo ya pwani," ilisema katika taarifa.

Mapema, watu wanaoishi katika maeneo ya pwani ya Mindanao ya Surigao Del Sur na Davao Mashariki nchini Ufilipino waliambiwa wahamie kwenye ardhi ya juu.

Baada ya tetemeko la kwanza la ardhi   , watu katika miji kadhaa walionekana wakikimbia kutoka kwenye majengo na kukaa katika maeneo ya wazi.