Jumatatu , 16th Mei , 2016

Serikali imesema ili kumuokoa mtoto wa kike kukatiza masomo yake kwa kupata mimba zisizotarajiwa itajenga mabweni katika maeneo ya jirani wanayosomea watoto hao pamoja na kuwashirikisha wazazi.

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo.

Akizungumza lBungeni mjini Dodoma wakati akiongezea mchango wa swali lililoelekezwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema serikali imepanga kutokomeza kabisa tatizo hilo linalokatiza ndoto za elimu ya watoto wengi wa kike nchini.

Mhe Jaffo amesema kuwa licha ya kujenga majengo hayo kwa ajili ya watoto wa kike lakini pia wanaanda mpango wa kuwa na nguvu ya pamoja na wazazi wa watoto hao ili kutokomeza tatizo hilo.

Naibu Waziri huyo amesema watoto wengi wanapenda kupanga mitaani kwa ajili ya kujisomea jambo ambalo linawafanya kuwa karibu na vishawishi vinavyowapelekea kujiiingiza katika mahusiano yanayoishia kukatiza ndoto zao.

Awali akijibu swali lililoelekezwa katika wizara yake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Hamisi Kigwangalla amewataka viongozi wote watilie mkazo katika halmshauri wanazotoka ili kumaliza suala hilo na si kusubiri kutoka serikali kuu pekee.

Sauti ya Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo