Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Tundu Lissu aikataza familia

Jumapili , 24th Sep , 2017

Familia ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, imesema imezuiliwa kuandika barua kwa ajili ya kuiomba serikali kugharamia matibabu ya mbunge huyo kwa madai amehaidi suala hilo atakuja kulishughulikia yeye mwenyewe hivi karibuni.

mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Hayo amebainisha kaka wa mbunge huyo ambaye pia ni msemaji wa familia, Alute Mughwai baada ya kupita siku kadhaa tokea serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kutoa kauli yao ya kusema mgonjwa ni mbunge ambaye anayehitaji matibabu zaidi lakini kwa kuwa yupo nje ya utaratibu wa serikali na ili serikali iweze kushiriki ni lazima yawepo maombi ya kufanya hivyo.

"Majira ya saa nne hivi niliweza kuzungumza na Mhe. Tundu Lissu akiwa hospitalini Nairobi baada ya kumjulia hali nilimueleza taarifa ya Mhe. Waziri kwamba tuandike barua ili aweze kupata matibabu kwa gharama za serikali, akanijibu kuwa jambo hilo atalizungumzia yeye mwenyewe siku za hivi karibuni. Kwa sababu yeye anaamini ni mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anahaki zote anazostahili kulipwa, kama mbunge ikiwa ni pamoja na kupatiwa matibabu endapo ataugua au atapatwa na maradhi", amesema Alute.

Pamoja na hayo, kaka wa Lissu ameendelea kwa kusema "Mpaka hivi sasa jeshi letu la polisi halijaweza kumkamata mshtakiwa yeyote juu ya tukio la Lissu wakati jambo hilo lilitokea mchana kweupe na watu wengi walishuhudia. Sasa mazingira hayo yametupa wasiwasi kama tukio hilo litachunguzwa kikamilifu, hatuna wasiwasi na uwezo wa polisi wetu kufanya huo uchunguzi lakini shida yetu ni utayari".

Aidha, Alute amesema wameshamuandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali ili waweze kupatiwa msaada wa kiuchunguzi zaidi dhidi ya tukio hilo lililomtokea ndugu yake.

"Barua tumeandika Septemba 16, mwaka huu kwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali maana ndiyo mamlaka inayopaswa kuchukua hatua za kuombwa msaada wa kiupelelezi kwa niaba ya serikali yetu huko nje ya nchi, na hiyo barua nimeinakili kwa Mhe. Waziri Sheria na Mambo ya Katiba", amesisitiza Alute.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa na risasi nje ya nyumba yake mjini Dodoma wakati akitokea Bungeni na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 na mwishowe kukimbiziwa katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita