Alhamisi , 8th Mei , 2014

Chama cha Msalaba Mwekundu leo (May 8, 2014) kimeadhimisha siku ya masalaba mwendu duniani ambapo kitaifa imefanyika mkoani Mbeya na kutakiwa kutumia wanafunzi katika utoaji wa huduma ya Kwanza.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Self Rashid amekitaka chama cha msalaba mwekundu nchini (Red Cross) kuwatumia vijana wanaosoma katika shule za msingi na sekondari kwa kuwapatia mafunzo ya utoaji huduma za kibinadamu ili huduma zitolewazo na chama hicho ziweze kuwa  endeleza na kuwafikia walengwa kwa wakati.

Waziri wa Afya Dkt. Self Rashid ametoa wito huo katika hotuba yake ambayo imesomwa na mkuu wa wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro kwenye maadhimisho ya siku ya chama cha msalaba mwekundu duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mbeya.

kwa upande wake makamu wa Rais wa chama cha msalaba mwekundu nchini ambaye pia ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Zainab Gama amesema chama cha msalaba mwekundu kimekuwa kikifanya kazi zake bila upendeleo kwa kutoa misaada ya kibinadamu wakati wa majanga,

Aidha mwenyekiti wa chama cha msalaba mwekundu mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili amesema chama cha msalaba mwekundu Tanzania kimekuwa ni chama cha kuigwa barani Afrika kutokana na chama hicho kutoa huduma zake kwa umakini kila huduma zake zinapohitajika