Akitangaza vikwazo hivyo Trump amesema mazungumzo yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin ya kumaliza vita vya Ukraine hayaendi popote.
Kwa miezi mingi, Trump amejizuia kuiwekea Urusi vikwazo, lakini uvumilivu wake ulifikia mwisho baada ya mipango ya kukutana na Putin huko Budapest kugonga mwamba.
'Trump anasema Jambo pekee analoweza kusema ni kwamba kila anapozungumza na Vladimir, wanakuwa na mazungumzo mazuri. Na kisha hayaendi popote.
Trump anasema muda umewadia wa kufikia makubaliano kwa sababu Watu wengi wanakufa,
Umoja wa Ulaya pia umetangaza vikwazo vipya kuishinikiza Urusi kumaliza vita vyake Ukraine ambavyo vimedumu kwa miaka mitatu na nusu sasa.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amepongeza vikwazo hivyo vipya vya Marekani na Umoja wa Ulaya, akivitaja kuwa ujumbe thabiti na unaohitajika zaidi kuishinikiza Urusi.

