Jumatano , 1st Nov , 2023

Askari Polisi kitengo cha Usalama Barabarani Sajenti Stella Alphonce, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari ya shule asubuhi ya leo Novemba 1, 2023 wakati akitekeleza majukumu yake ya ukaguzi barabarani katika eneo la Nyamuhongolo Jijini Mwanza.

Basi lililomgonga Trafiki

Akieleza kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa,  amesema Askari huyo alisimamisha gari hilo kwa ajili ya ukaguzi, baada ya gari kukutwa na kosa na alimtaka dereva arudishe nyuma gari kwa ajili ya usalama, ndipo alimgonga askari huyo kwa nyuma na kusababisha kifo chake.

Hata hivyo Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limesema linamshikilia dereva wa gari hiyo ya shule ya msingi Nyamuge, Philipo Mhina kwa kutenda kosa hilo.