Prof.Mohamed Janabi, Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi, kwenye maadhimisho ya siku uchangiaji viungo Duniani leo Hospitalini hapo.
"Bado tunatumia watu walio hai lakini siku zijazo tuna mpango wa kupendekeza hata waliokufa tuchukue figo zao tupandikizie watu ili kutanua wigo wa upandikizaji Figo nchini", alisema Prof. Janabi.
Aidha anataja takwimu za wagonjwa sugu wa Figo nchini.
"Hapa nchini takribani asilimia 7 ya watu wana ugonjwa Sugu wa Figo, na niseme tu kusafisha Figo ni daraja la kupandikizwa figo, na ukishapandikizwa unaondokana na usafishaji wa mara kwa mara ambao ni gharama"alisema Prof. Janabi.
Leo Tanzania na mataifa mengine yanaungana katika maadhimisho ya siku ya Figo Duniani, hawa hapa ni baadhi ya watu waliotoa na kupandikzwa Figo hapa nchini.
"Mimi nilmtolea Figo mwanangu tangu mwaka 2019 na mpaka leo nipo vizuri sina tatizo llote na mwanangu mpaka sasa ana watoto na anaendelea na maisha yuake kama kawaida", alisema Juma Omary, Mchangiaji wa Figo .
"Nina miaka 10 toka nipandikizwe Figo naishukuru Serikali ilinigharamia kwenda India kufanyiwa upandikizaji na alienitolea figo anaendelea na maisha yake, niwaambie watanzania wenzangu msiogope kuchangia ndugu zenu", alisema Zenobias Bikoga, Aliepandikizwa Figo.
"Figo zangu zote mbili zilifeli nikaanza kusafisha lakini baadae Rais magufuli akatoa msaada wa kupandikizwa na tulikuwa watano tunapandikizwa na mpaka leo tupo hai tunaendelea na maisha yetu hakuna changamoto yeyote tunapitia", Alisema Rehema Mongo, Aliepandikizwa Figo.