Jumapili , 5th Dec , 2021

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro ameendesha oparesheni ya mazao wilayani Tunduru kwa siku 2 mfululizo na kufanikiwa kukamata tani 10 za korosho zilizooza za miaka ya nyuma ambazo hazizalishwi wilayani Tunduru.

Sehemu ya Korosho zilizokamatwa

DC Mtatiro ameiongoza Kamati ya Usalama ya Wilaya yake kufanya oparesheni hiyo baada ya kujulishwa kuwepo kwa njama za baadhi ya wafanyabiashara wenye nia ovu ya kuingiza korosho chafu na zilizooza kwenye soko la korosho bora inayozalishwa wilayani Tunduru.

Katika oparesheni iliyoisha Ijumaa  saa 8.30 usiku, jumla ya tani 10 za korosho na watuhumiwa 6 walitiwa mbaroni.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro akiwa na mmoja wa watuhumiwa.

Mtatiro amesema taratibu zote zikikamilika korosho hizo zilizooza na zisizofaa zitateketezwa kwa mujibu wa sheria ili wajanja wasije kuziingiza sokoni.